Handbook

Jarida la Ustawi

summary

Jarida hili la ustawi ni matokeo ya na ushirikiano na wanawake katika siasa , wanawake watetezi wa haki za binadamu na wataalamu wa afya ya akili kote Ivory Coast na Tanzania. Jarida hili litatumika kuonesha uzoefu wao wa maisha kama wanasiasa na viongozi wanaopitia mambo mbalimbali katika kazi zao, kwa kuzingatia changamoto zilizo wakati wa uchaguzi wa 2025 katika mataifa yote mawili. Kwa kuchanganya uzoefu katika kutafuta suluhisho kutoka kwa viongozi wanawake na wabobevu wa wataalamu wa afya ya akili, jarida hili linatoa mikakati thabiti na ya vitendo ya usimamizi wa afya vya akili na kipaumbele cha ustawi katika maisha ya kila siku. Mchakato wa maendeleo uliratibiwa kimkakati na Pollicy kwa ushirikiano na Leadafricaines, Faraji H Emily, na Dkt. Nour Bakayoko. Ushirikiano wao wa dhati katika kutekeleza mradi, ukusanyaji wa data, na uundaji wa zana hii ya ustawi ulikuwa wa thamani kubwa, ukiimarisha sana mchakato na matokeo ya mwisho. Ushirikiano huu ulikuwa muhimu katika kuhakikisha mkakati wetu unabaki imara katika kutekeleza maono ya Pollicy: kutumia data kuwapa na kuwawezesha wanawake kufanya maamuzi sahihi na kuendeleza haki ya kijamii, huku ustawi wa pamoja na wa mtu binafsi ukiwa kipaumbele. Tunatoa shukrani za dhati kwa wadau wote waliochangia kupitia mahojiano, warsha, na mafunzo, na kwa kushiriki kwa ukarimu masimulizi yao binafsi. Shukrani maalum ziende kwa wanachama wa Mitandao yetu ya Usaidizi; Réseau huko Ivory Coast na Bega la dada nchini Tanzania, ambao mshikamano wao usioyumba ni msingi wa kazi hii na unaendelea kudumu baada ya chapisho hili. Hatimaye, tunawashukuru wakaguzi wa kitabu hiki na timu iliyojitolea ya Pollicy kwa maoni na mwongozo wao wenye ufahamu. Michango yao imekuwa ya muhimu katika kuboresha na kukamilisha jarida hili la ustawi kuwa rasilimali imara na ya vitendo katika kujenga usalama na ustawi.