Deprecated: Creation of dynamic property FusionSC_Column::$is_nested is deprecated in /home2/pollicyo/public_html/archive/wp-content/plugins/fusion-builder/inc/class-fusion-column-element.php on line 551

Deprecated: Creation of dynamic property FusionSC_FusionText::$params is deprecated in /home2/pollicyo/public_html/archive/wp-content/plugins/fusion-builder/shortcodes/fusion-text.php on line 126

Haki za Kidijitali ni Haki za Wanawake!

Mwongozo wa rasilimali unaosaidia wanaharakati na mashirika ya haki za wanawake kushiriki katika harakati za haki za kidijitali.

Utangulizi

Haki za Kidijitali ni zipi?

Picha ya mwanamke aliyesuka mabutu na  kuvalia vazi la kitenge akifanya kazi kwenye kompyuta yake mpakato na akiandika kumbukumbu. Picha: Neema Iyer

Tunaweza kuzielezea haki za kidijitali kama haki za (binadamu) zinazotumika katika mazingira ya kidijitali. Hii inamaanisha matumizi ya moja kwa moja na uhamishaji wa haki za binadamu kama ilivyo ainishwa chini ya maazimio kama Azimio la Haki za Binadamu [1] (UDHR) ili kudumisha utu na usawa wa watu kila mahali huku ukijumuisha nafasi za kidijitali.

Nafasi za kidijitali au mtandaoni hazimaanishi tu nafasi za mtandao kama vile majukwaa ya mitandao ya kijamii na mijadala kama Facebook, Twitter au Instagram au masoko ya mtandaoni, blogi na wavuti binafsi bali pia mazingira ambayo yanawezesha mwingiliano kati ya watu na teknolojia. Hii inaweza kujumuisha programu kama vile jokofu za kisasa, ‘fitbits’, kamera za ufuatiliaji na programu ya biometriska.

Nafasi za kidijitali au mtandaoni hazimaanishi tu nafasi za mtandao kama vile majukwaa ya mitandao ya kijamii na mijadala kama Facebook, Twitter au Instagram au sehemu ya masoko mtandaoni, blogi na wavuti za binafsi, lakini pia kwa mazingira ambayo yanawezesha mwingiliano kati ya watu na teknolojia.

Wakati neno “teknolojia” lenyewe hutumiwa mara kwa mara na “dijitali”, ni muhimu kutambua kuwa teknolojia za dijitali pia ni moja ya aina nyingi za teknolojia zinazotumika leo. Kwa hivyo, wakati neno “dijitali” linaweza kupotosha, njia muhimu zaidi ya kuangalia aina ya haki tunazo rejelea ni kufikiria juu ya aina zote za haki za binadamu zilizo kamilishwa au kufanywa kuwa muhimu kama matokeo ya mwingiliano wetu unaojulikana na usiojulikana na teknolojia ya dijitali.

CHANGAMOTO

Leo baadhi ya changamoto kubwa katika haki za kidigitali ni pamoja na udhibiti wa serikali na majukwaa ya mtandao. Kwa mfano, katika 2019, Shirika la Ushirikiano wa Sera ya Kimataifa ya TEHAMA katika Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (CIPESA) iliripoti [2] kuwa kutoka 2016 hadi 2019, zaidi ya nchi ishirini (20) za kiafrika ziliamuru kufunga kwa mitandao kuzuia watu kutoka nchi hizo kupata tovuti maarufu za mitandao ya kijamii na wakati mwingine kuzuia UJUMBE MFUPI (SMS) na huduma za pesa za rununu.

Vivyo hivyo, kote Afrika kumekuwa na majaribio mbalimbali, mengine yamefanikiwa na mengine hayajafanikiwi, kupitisha miswada moja kwa moja kupunguza uhuru wa kujieleza kwenye mitandao ama kwa kulazimisha watumiaji wa mitandao ya kijamii na wamiliki wa majukwaa kujisajili au kuchukuliwa hatua za uhalifu wa wapinzani kwa kuiona kama tishio la usalama kwa taifa.

Majukwaa ya mitandao ya kijamii yenyewe katika kujaribu kuzuia kuenea kwa lugha za chuki na habari potofu yameanza kutegemea zaidi zana za kuchuja za kiotomatiki.

Licha ya zana kuelezewa kuwa zinakabiliwa na matokeo ya uwongo. Hii inamaanisha kuwa zana za kiotomatiki huweka lebo kwenye maudhui kama ya vurugu au habari potofu wakati inaweza kuwa sivyo. Hivyo, wastani wa maudhui kiotomatiki iliyotengenezwa na kampuni za teknolojia hayawezi kuwa na ustadi mkubwa na hivyo kupelekea kuzuia haki ya kujieleza.

Changamoto nyingine zinazokumba haki za kidijitali leo ni kuongezeka kwa watumiaji wa utambuzi wa uso na mifumo mingine ya ufuatiliaji wa watu wengi kuchunguza watu.

Hii ni ukiukaji wa faragha vilevile utu. Mifumo ya utambuzi wa uso imekuwa ikihusishwa mara nyingi na dosari katika kubaini watu weusi na kusababisha kufungwa na kukamatwa kimakosa. Mifumo hii hutengeneza mazingira tulivu ya uhuru wa kidemokrasia na kuzuia watu kutumia haki zao za kidijitali mtandaoni na mara nyingi hupelekea hufanya uhalifu wa haki hizi.

Ugumu unaowakumba  watu wengi leo katika kutumia intaneti kupitia simu zao za mkononi au kompyuta pia ni kizuizi kwa utekelezwaji kamili wa haki za dijitali. Suala hili linachangiwa na miundombinu, uchumi na sababu za kitamaduni.

Matokeo Chanya ya Teknolojia kwa Wanawake

Picha ya mwanamke aliyevaa fulana ya rangi ya machungwa, kitenge na hijab ya zambarau akitabasamu wakati akiangalia kitu kwenye simu janja. Akiwa sokoni. Picha: Neema Iyer

Kwa wanawake wengi, ujio wa teknolojia kama vile intaneti ni njia mpya na fursa ya kushiriki katika mazungumzo na kutetea mahitaji yao. Maendeleo ya kiteknolojia hutoa majukwaa makubwa bila (Vi) zuizi vyovyote vya kitamaduni na uchumi vilivyoundwa dhidi ya wanawake na fursa nyingine zenye kuwaletea hamasa. Kama ongezeko la uanaharakati wa kidijitali linavyoonesha, mtandao huongeza ufahamu wa masuala muhimu ambayo huleta manufaa kwa wanawake kuwa rahisi kutimiza. Wanawake hutumia nafasi hizi kuelezea vipaji vyao na ubunifu, kukuza kazi zao na biashara na vile vile kuwasiliana na kujenga urafiki mpya.

Ubunifu wa teknolojia hutoa suluhisho kwa wanawake na kuwasaidia katika kutekeleza majukumu ya kila siku. Matumizi ya teknolojia kwa sekta na viwanda vingi imeunda vituo vingi vya kusaidia kama kifedha-teknolojia, afya-teknolojia, masoko -teknolojia, elimu-teknolojia, suluhisho la kilimo-teknolojia ambazo husaidia wanawake wengi ulimwenguni leo kutimiza shughuli zao kwa ufanisi zaidi.

Ulinzi Mtandaoni

Nafasi za mtandaoni mara nyingi huficha na kuendeleza vitisho kwa wanawake husika. Wanawake wanaathiriwa vibaya na vurugu za mtandaoni kama vile unyanyasaji wa kijinsia unaotokana na za ngono[3] usambazaji usiofaa wa picha za faragha pia utapeli wa mtandaoni na kudukuliwa.

Wanawake wamebainika kuwa na uwezekano wa picha zao za mahusiano kusambazwa mtandaoni bila idhini yao mara mbili zaidi ya wanaume  [4]. Ukosefu wa suluhisho unaotumia njia ya kijinsia kuhusu uchochezi mtandaoni na uhalifu umefanya iwe ngumu kwa wanawake kutafuta msaada kutoka kwa mamlaka za serikali na binafsi.

Ripoti ya 2020 ya Plan International iliyojumuisha wasichana na wanawake wenye umri mdogo 14,000 kutoka nchi 31 ilionesha kwamba 58% ya washiriki wamenyanyaswa au kudhalilishwa mtandaoni [5]. Vivyo hivyo, matokeo kutoka kwa ripoti yetu ya 2020, ***Alternate Realities, Alternate Internets***, ilionesha kwamba 1 kati ya wanawake 3 waliohojiwa katika nchi zetu tano za utafiti kote Afrika wamepata aina fulani ya unyanyasaji wa kijinsia mtandaoni, na unyanyasaji wa kijinsia ulikuwa asilimia 36 ya udhalilishaji mtandaoni zilipatikana [6].

Habari potofu, Upotoshaji na habari Mbaya

Habari potofu, habari isiyo sahihi na habari mbaya pia ni mifano ya vitisho vikubwa vya kidijitali kwa wanawake. Ingawa habari potofu inahusu kushiriki kutuma habari za uwongo au za kupotosha, habari isiyo sahihi ni habari potofu na habari mbaya ni utumiaji wa habari ya kweli na sahihi kwa makusudio ya kudhuru [7].

Habari potofu, habari isiyo sahihi na habari mbaya ni aina ya vurugu za mtandaoni ambazo zina asili ya jinsia tofauti na ambayo mara nyingi hulenga wanawake mashuhuri katika siasa, uandishi wa habari na wanaharakati wa haki za wanawake kuwadharau [8].

Mashambulio haya mara nyingi ni ya kijinsia, yanaweza kutumia aina ya vyombo vya habari kama vile dipufeksi [9] na mara nyingi hutumia safu kadhaa za shambulio la kibinafsi dhidi ya jinsia na ujinsia kwa Wahadhiriwa waliokusudiwa. Habari zenye mlengo wa kuleta vurugu mara nyingi huwa zenye uwongo au hofu iliyopo tayari na kuipitisha ionekane ya ukweli. Kama matokeo, habari potofu, habari isiyo  na habari mbaya hutoa vitisho vikali kwa taasisi za kidemokrasia nyakati za sasa [10].

Upatikanaji

Picha ya mtoto mchanga aliye na mavazi ya rangi ya mnanaa, akicheza na kompyuta mpakato. Picha: Neema Iyer.

Kutokana na ripoti ya Umoja wa Kimataifa ya Mawasiliano (ITU) mwaka 2019 [11], ni asilimia 48 tu ya wanawake wanaotumia mtandao, ikilinganishwa na asilimia 58 ya wanaume ulimwenguni. Ripoti hiyo pia inasema kwamba idadi ya wanawake wanaotumia mtandao ni kubwa kuliko ile ya wanaume katika asilimia 8 tu ya nchi, na usawa wa kijinsia katika utumiaji wa mtandao hupatikana tu katika zaidi ya robo moja ya nchi.

Uchunguzi mwingine kama vile wa Jumuiya ya Wavuti [12] pia unaonyesha kuwa wanaume hubaki asilimia 21 zaidi kuliko wanawake kuweza kuwa mtandaoni, idadi ikiongezeka hadi asilimia 52 katika nchi zilizoendelea zaidi duniani (LDCs). Ripoti ya GSMA juu ya Mgawanyiko wa Jinsia ya Dijitali inaweka pengo la jinsia ya rununu katika nchi za chini ya Jangwa la Sahara kwa asilimia 37, idadi ambayo inajulikana kuwa ya pili kwa juu zaidi ulimwenguni [13].

Baadhi ya sababu zinazo zuia upatikanaji wa mtandao kwa wanawake ni kutoka kwa vizuizi vya kitamaduni, kiuchumi na miundombinu vianyoathri hadi wakati huu, uwezo wa kununua, ujuzi wa kidijitali, ubora wa huduma na vizuizi vya upatikanaji.

Mgawanyiko wa kijinsia wa kidijitali kwa hivyo pia umefungwa na pengo la kijinsia na pia mfumo kandamizi. Wanawake, ambao mara nyingi ni walezi wa kimsingi katika nyumba zao wanatarajiwa kufanya kazi ya nyumbani isiyolipwa ambayo hutumia muda wao na mapato na kuwaacha hawana njia au fursa ya ushiriki mtandaoni. Upendeleo uliomo katika maendeleo ya teknolojia na usambazaji na utamaduni pia huzuia wanawake kuwa watumiaji wa mwanzo teknolojia.

Kuzimwa kwa Mtandao

Baadhi ya visingizio ambavyo vimetajwa [14] kama haki ya kufungwa kwa mtandao na serikali ni pamoja na kuzuia udanganyifu wa wanafunzi wakati wa mitihani ya kitaifa, kukandamiza ripoti, kukosoa au kupinga wakati wa uchaguzi au maandamano au karibu na kupiga marufuku kuenea kwa habari kuhusu mashambulizi ya kigaidi, hata kuripoti taarifa sahihi, ili kuzuia hofu na viashiria vya vurugu.

Kuzimwa kwa mtandao kumeonyeshwa kuathiri vibaya watu kama wanawake, haswa wakati wa mazingira magumu ambayo hutokea kuathiri wanawake wa vijijini kutokana na sababu za umaskini na ukandamizaji wa kijinsia. Jamii ndogo za kikabila huhisi kutengwa wakati wa kuzima mtandao.

Ripoti [15] juu ya athari za kuzimwa kwa wavuti ya wanawake huko Manipur, India, iliorodhesha hasara za kiuchumi, usalama, uhuru wa kuzungumza, ustawi wa kihisia, hakuna msaada kutoka kwa serikali wa hali ya dharura kama athari zingine za majanga ya kufungiwa kwa wanawake.

Kuzimwa kwa mtandao pia kunaathiri wanaharakati ambao wanategemea mtandao kufanya mawasiliano na washirika wa ndani na wa kimataifa na wadhamini na pia raia. Katika nakala ya Chama cha Mawasiliano ya Maendeleo [16], juu ya athari za kuzimwa kwa wavuti barani Afrika, Françoise Mukuku, mwanaharakati wa haki za dijitali na mkurugenzi mtendaji wa zamani wa Si Jeunesse Savait, shirika la wanawake vijana la makao makuu nchini DRC alielezea hisia katika maneno yafuatayo:

"Ni kama kukatwa kutoka ulimwenguni. Kuchanganyikiwa kwa kutokujua ni lini itarudi, iliongezeka na masaibu ya kuwa na simu ya rafiki yako anaeishi huko Ulaya, kuwapa nywila yako ili waweze kupata barua pepe yako kwa niaba yako na kupata nambari ya simu zako za mawasiliano muhimu sana. Unaumia kwa uchungu, kwa sababu huwezi kumaliza kazi kufikia tarehe za mwisho wa kazi zako."

Hisia ya kukosa nguvu na kukatwa kwa mtandao ni jinsi mtu mwingine aliyejibu, Arsene Tungali, mkurugenzi mtendaji wa Rudi International alielezea kuzima:

"Unampigia simu rafiki zako kuwauliza ikiwa wanaweza kuunganishwa na mtandao, wanakuambia walitaka kukupigia simu pia kuangalia kama una mtandao. Unagundua kuwa mtandao umezimwa na ni kama unarudi nyuma kama karne kumi zililopita, ulimwengu unasimama mbele yako kwani huwezi kusoma barua pepe zako, hauwezi kuangalia ujumbe wako wa WhatsApp, hauwezi kuvinjari kwenye mitandao yoyote ya kijamii. Inasikitisha sana. Unajisikia kukosa nguvu na kudhoofishwa na wale ambao wana nguvu."

Katika kipindi cha janga, kama hili la korona, ni muhimu kwa mifumo ya mawasiliano wazi kuwapo imara na salama. Majukwaa ya dijitali hutengeneza fursa za elimu na ustawi juu ya maswala kama vile afya ya ujinsia na uzazi na elimu ya kifedha ambayo inaweza kuwa vizuizi kwa wanawake na kwa hivyo wakati inawezekana kwa wanaume na wavulana wadogo kuendelea na masomo yao au biashara, wanawake hukatazwa na wanashindwa kufanya hivyo [17].

Ufuatiliaji

Picha ya uso wa mwanamke mwenye nywele nyeusi za afro. Kwenye uso wake kuna muhtasari wa mistari na nukta zinazotumiwa katika teknolojia ya utambuzi wa uso. Akiwa ufukweni. Picha: Neema Iyer

Matumizi ya mifumo ya ufuatiliaji na watu binafsi, mara nyingi jamaa wa kiume na wenzi wao na maajenti wa serikali kufuatilia shughuli za wanawake ni aina ya unyanyasaji una wezeshwa na teknolojia – ambayo ni unyanyasaji unaofanywa kwa msaada wa aina yoyote ya teknolojia, pamoja na lakini sio mdogo kwa teknolojia ya dijitali na mtandaoni – dhidi ya wanawake wanaokiuka haki zao za dijitali. Mbaya zaidi, kwa sababu wanawake mara nyingi hawajui sana masuala ya dijitali, wanaweza kuwa hawajui usanikishaji na utumiaji wa vifaa hivi na vile vile jinsi ya kuzima.

Ufuatiliaji unaofanywa kwa wanawake mara nyingi huchukuliwa kama wenye faida kwa usalama wa wanawake hata hivyo, ukiukaji huu wa faragha umekuwa ukitajwa kuwa aina ya unyanyasaji dhidi ya wanawake walio tumiwa kudhibiti [18], unyanyasaji na kulazimisha wanawake kutii mamlaka za chini kupitia mawakala wa umma na kibinafsi kwa niaba ya jamii yenye mfumo dume.

Ufuatiliaji wa wanawake huzuia kuwa na uhuru wa kujieleza na hairuhusu wanawake kuwa kama watu huru walio na uhuru binafsi.

Uamuzi wa Teknolojia

Uamuzi wa teknolojia unamaanisha wazo kwamba teknolojia (ubunifu), na sio watu, wanahusika na mabadiliko ya kitamaduni yanayosababishwa na teknolojia kwa watu na jamii pia. Kutokana na Ruha Benjamin, uamuzi wa teknolojia unaweka teknolojia kwenye kiti cha dereva. Kwa msingi wake, uamuzi wa teknolojia unakuza wazo kwamba teknolojia ni nguvu inayo jitegemea, na kwamba athari za kupelekwa na matumizi yake, yenye faida au la, hayaepukiki.

Barani Afrika, uamuzi wa kiteknolojia umeathiri mijadala inayozunguka utekelezaji wa miundombinu ya TEHAMA. Inachukuliwa kama kawaida katika visa vingi, kwamba TEHAMA itabadilisha uchumi wa mataifa mengi ya Kiafrika na uraia wao. Majadiliano haya mara nyingi hufanywa bila kuzingatia hali na sababu za kijinsia ambazo zinahakikisha kuwa wanawake wananyimwa kupata teknolojia hizi. Athari hii pia inatokea kwa mfumo wa kiotomatiki wa kazi zenye ujuzi wa chini ambazo mara nyingi hufanywa na wanawake.

Kupitishwa kwa azimio la mfumo wa kiotomatiki na wana uchumi wa ulimwengu kwa matumaini ya ukuzaji wa uchumi wa kitaifa kwa hivyo hupuuza athari kwa wanawake na kuweka uwezo wao wa kushiriki katika nafasi za dijitali kuwa hatarini [19].

Nchini Nigeria [20] na pia nchi zingine, barani Afrika [21], ukuaji wa haraka wa tasnia ya fintech na huduma wanazotoaNchini Nigeria zimesababisha kuendelezwa kwa mazoea ya ukusanyaji wa data unaozidi kuingilia kwa madhumuni ya kupata faida, ambayo yanahesabiwa haki kama hatua isiyoepukika katika utekelezaji wa jamii ya dijitali.

Walakini, hii haingeweza kuwa mbali na ukweli kwani teknolojia sio nguvu ya kujiendesha lakini moja ya sababu ya mvutano kati ya wadau mbalimbali.

Ujenzi wa harakati

Je! Vikundi vya Wanawake na Haki za Wanawake vinawezaje kushiriki katika Harakati za Haki za Dijitali?

Picha ya mwanamke aliye na kitambaa cha bluu kichwani, shoal nyekundu, na vito vya thamani akiangalia kwenye simu yake ya kisasa. Yupo kwenye mkutano wa kikundi cha wanawake. Picha: Neema Iyer

Changamoto ambazo wanawake wanakabiliwa nazo katika nafasi za dijitali leo hutoa fursa kwa vikundi vya wanawake na haki za wanawake kushiriki, kushirikiana na kutatua changamoto kandamizi inayo wezeshwa na teknolojia na kuendeleza haki za wanawake mtandaoni.

Wakati harakati za watetea haki za wanawake na wanawake wenyewe mara nyingi zimefungwa au kutumika kwa kubadilishana kumaanisha kitu kimoja, watafiti wa kike [22] wamejitahidi kuweka alama ya tofauti kati yao. Ufafanuzi mmoja uliopendekezwa ni kwamba harakati za haki za wanawake zinaweza kufafanuliwa kama sehemu ndogo ya harakati za kijamii na kisiasa kwa kuzingatia uzoefu wa kijinsia wa wanawake. Uzoefu huu unaweza kuwa wa kiuchumi kwa asili, kwa hivyo kusaidia fursa za uwezeshaji wa kifedha kwa wanawake, kisiasa, ili kuboresha muonekano wa wanawake katika nafasi ya kisiasa, na hata wazalendo kwa asili.

Ufafanuzi mwingine hufafanua harakati za wanawake kujumuisha hata harakati za kike na harakati za kupinga harakati za wanawake lakini ina eleza tofauti kati ya harakati za wanawake na wanawake katika harakati, ikifafanua mwisho huo kuwa na maana ya ushiriki wa wanawake katika harakati zingine za kijamii [23]. Harakati za wanawake, hata hivyo, zinajulikana hasa na changamoto zao katika miundo ya mfumo dume.

Harakati za wanawake zimekosolewa kwa wakati mwingine kutafuta kudumisha majukumu ya jadi yanayoshikiliwa na wanawake, kama kuzaa watoto na kuhudumia familia. Walakini, licha ya changamoto hizi, harakati za wanawake zinafaa sana katika kusisitiza na kukuza na kutetea haki za wanawake katika sekta muhimu.

Makundi mengi ya watetezi ya wanawake leo wanaelewa thamani ya kuandaa mtandaoni na katika nafasi za dijitali haswa kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya ujumbe kama vile WhatsApp, Facebook na Twitter. Harakati za haki za dijitali, ambazo zinajumuisha harakati zote za wanaharakati ambazo zinaenea tu na kuwezeshwa kupitia nafasi za mtandaoni na pia maswala yanayohusiana moja kwa moja na haki za dijitali, zinaweza kutumia vifupisho kama hashtag. Mifano ya mafanikio ya harakati za mitandao ya kijamii kama vile: #MeToo, #EndSars, #BlackLivesMatter, #CongoIsBleeding, #ShutItAllDown, and #KeepItOnUganda imeonyesha kwa nguvu jinsi harakati za haki za binadamu zinaweza kupigwa na kuletwa mbele kwenye mtandao.

Kuongeza Ufahamu

Sehemu ya msingi uliofanywa na vikundi vya harakati za wanawake kuhusu maswala ambayo yanaathiri wanawake kipekee ni kukuza uelewa katika jamii na katika ngazi ya mkoa au kitaifa kupitia mikutano ya kumbi za mjini na viongozi wa mitaa na wanawake, ufikiaji wa maeneo ya kidini ya ibada, shule na maeneo ya umma. Shughuli hizi zinaweza kusaidiwa na vipeperushi, mabango, maonyesho ya maigizo na hotuba.

Lengo la kukuza uelewa ni kueneza habari na kuleta uelewa wa athari kwa vitendo, ambayo katika kisa hiki itakuwa mazoea ya kawaida ambayo yanaathiri haki za dijitali za wanawake.

Wakati uhamasishaji mtandaoni ni muhimu sana, kufanya kazi tu katika nafasi za mtandaoni kunaweza kudanganya na kupotosha vikundi vya wanaharakati juu ya ufanisi wa kampeni zao. Lengo la jumla la kampeni za uhamasishaji hatimaye husababisha mabadiliko katika fahamu ya pamoja ya jamii. Kwa bahati nzuri, vikundi vya harakati za wanawake na haki za wanawake kihistoria vimefanikiwa kuandaa, mihadhara ya kuonana na ya kimtandao, kupinga hali iliyopo.

Nchini Uganda kwa mfano, Mtandao wa Wanawake wa Uganda (WOUGNET), walifanya kampeni na hashtag hiyo #SayNoToOnlineGBV kwa muda wa Siku 16 za Uanaharakati dhidi ya UWAKI mnamo 2020, pamoja na Encrypt Uganda, DefendDefenders, Maabara ya Haki za Binadamu ya Dijitali, Watetezi wa Afrika na Mpango wa Usomaji wa dijitali unaangazia maswala na kesi za UWAKI mtandaoni nchini Uganda. WOUGNET iliangazia aina zilizotambuliwa za unyanyasaji wa kijinsia mtandaoni kujumuisha: picha za ngono zisizo na ridhaa, unyanyasaji wa mtandaoni, unyanyasaji wa kingono mtandaoni, doksia, kutumia mtandao, na uigaji [24].

Picha ya 1: Picha ya skrini ya kampeni ya Mtandao wa Wanawake wa Uganda #SayNoToOnlineGBV

Picha ya 2: Picha ya skrini ya kampeni ya  WiLDAF-TZ#WanawakenaMtandao

Katika kipindi hicho hicho, Kituo cha Teknolojia ya Habari na Maendeleo (CITAD) kiliandaa shughuli kadhaa, mtandaoni na nje ya mtandao, juu ya haki na hatari za dijitali na ikatengeneza jarida la unyanyasaji mtandaoni kwa wanafunzi wa kike katika shule za sekondari [25].

Utetezi na Mabadiliko ya Sera

Mara nyingi, kufuatia mafanikio ya kampeni za kukuza uelewa na wakati mwingine kwa kushirikiana nao, vikundi vya wanawake na vya kike huunda kuhusu maarifa ya pamoja kutetea mabadiliko ya kijamii na utamaduni na kisheria. Sheria na sera zinahitaji msaada na makubaliano ya watu ili kufanikiwa na kutekeleza kwa ufanisi malengo yao yaliyokusudiwa.

Utetezi pia unaweza kuhusisha kushirikiana na vikundi vingine vya haki za kijamii ili kuongeza hatua za kukabiliana na kuongezeka kwa athari. Mabadiliko ya sera yanayotarajiwa yanaweza kuandaliwa kutoka ngazi za serikali za mitaa hadi ngazi za jimbo au za mkoa kabla ya athari kubwa kuonekana. Inaweza pia kuwa njia nyingine na kuanzia katika ngazi ya kitaifa.

Katika Jamhuri ya Benin, Mylène Flicka, mwanaharakati wa Benin anayefanya kazi na wanaharakati wengine waliofanikiwa kupigania kumaliza ushuru wa mitandao ya kijamii ilianzishwa na serikali ya Benin ambayo ingeweza kupunguza idadi ya wanao tumia njia ya mtandaoni kwa asilimia 20 [26].

Kwa kuunda maombi na hashtag, #TaxePasMesMo (Usilipe kodi megabytes zangu), pamoja na maandamano ya nje ya mtandao na kukaa ndani, Mylène na wanaharakati wengine na vikundi viliweza kufanikiwa kuishinda serikali ya Benin hivyo kufutilia mbali ushuru huo. Kwa Pollicy, tumebuni mwongozo kwa mashirika yanayopenda utetezi wa haki za dijitali [27].

Image 3: Scrinishoti ya mwito wa Mylène Flicka #TaxePasMesMo

Kusaidia Wanawake katika STEM

Sio habari kwamba licha ya historia ya wanawake katika teknolojia, na msimbi wa kwanza alikuwa mwanamke, Ada Lovelace na michango muhimu ya waandaaji wa wanawake katika Vita vya pili ya Kidunia, leo tasnia ya teknolojia inatawaliwa sana na wanaume. Takwimu zinazoonyesha [28] kwamba asilimia 25 ya wafanyakazi wa Google, Apple, Facebook, Amazon na Microsoft ni wanawake na ni asilimia 37 tu ya waanzilishi wa teknolojia wana angalau mwanamke mmoja kwenye bodi ya wakurugenzi. Ripoti hiyo pia inaonyesha uwiano wa wanaume na wanawake kama 5:1!

Sehemu muhimu ya kukuza haki za dijitali ni kwa kubadilisha mazingira ya kijamaa ambayo ubunifu mwingi wa teknolojia umeendelezwa. Hii inaweza kufanywa kwa kusaidia na kuhamasisha wasichana na wanawake wadogo katika uwanja wa STEM na STEM- filidi zingine. Walakini, kazi haiishii hapo. Imeonyeshwa kuwa asilimia 41 ya wanawake katika STEM wameacha kazi zao wakati tu asilimia 17 ya wanaume hufanya hivyo. Kusaidia wanawake katika STEM ni mchakato endelevu ambao unajumuisha idadi kubwa ya wadau kuhakikisha kuwa wanawake wanaoingia uwanja huu wanakaa na kushamiri vizuri vya kutosha kuwatia moyo wanawake wengine.

Mfano mmoja wa mtandao kama huo ni WanaData [29], mtandao wa Pan-African wa wanasayansi wa data za kike na wanasayansi wanaotumia uandishi wa habari ili kubadilisha mazingira ya kuripoti habari barani Afrika. Mfano mwingine mzuri ni Django Girls, shirika lisilo la faida duniani na jamii inayowapa nguvu na kuwasaidia wanawake kuandaa warsha za bure, za siku moja kwa kutoa mafunzo, rasilimali na msaada. Tangu 2014, hafla za wasichana wa Django zimefanyika katika miji 534 katika nchi 98 [30].

Picha ya 4: Ukweli juu ya Mpango wa AkiraChix’s codeHive ulioko Nairobi, Kenya

Takwimu na Mipango ya Kusoma kwa Dijitali

Ingawa sio wanawake wote wanaweza – au wanapaswa! – kwenda kwenye uwanja wa STEM, ulimwengu wa leo wa dijitali hufanya iwe muhimu kwa kila mtu kuwa na ustadi wa kusoma kidijitali. Ni muhimu kwa wanawake kuweza kuwasiliana na kujenga ulimwengu wa mawazo yao wenyewe kidijitali. Ili kudhibiti maisha yao ya kidijitali, wanawake pia wanahitaji kuwa na uwezo wa kudhibiti au angalau kufuatilia matumizi yao ya data ili kuhakikisha inatumika kwa madhumuni ya faida.

Programu zilizofanikiwa kufundisha wanawake katika usalama wa dijitali ni pamoja na Safe Sisters au Dada Salama, mpango wa ushirika ambao hufundisha watetezi wa haki za binadamu wanawake, waandishi wa habari au wafanyakazi wa mitandao, na wanaharakati kuelewa na kujibu changamoto za usalama wa kidijitali wanazokabiliana nazo katika kazi zao na maisha yao ya kila siku. Cyberwomen [32] na Tactical Tech’s Gender and Tech Resources Wiki [33] ni mifano mingine ya programu zilizo na mitaala ya usalama wa dijitali inayolenga kuwapa wakufunzi zana za kutoa uzoefu wa kujifunza moja kwa moja ya mtu kwa watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi.

Kwa kushirikiana na vikundi hivi, mashirika ya watetezi wa haki za wanawake yana uwezo wa kushiriki uzoefu unaofaa wa kijinsia na data na kutoa ushauri wa kudumu [34].

Picha 5: Safe Sisters Digital Hygiene Guide

RASILIMALI

Hapa kuna orodha kadhaa za kusoma ili uanze juu ya mambo yote haki za dijiti!

MACHAPISHO YALIYOTUMIKA

  1. “Universal Declaration of Human Rights,” United Nations, accessed February 23, 2021, https://www.un.org/en/universal-declaration-human-rights/.
  2. CIPESA, Digital Rights in Africa- Challenges and Policy Options (Kampala: CIPESA, 2019), 5, accessed February 23, 2021, https://cipesa.org/?wpfb_dl=287.
  3. Sophie Maddocks, “‘Revenge Porn’: 5 Important Reasons Why We Should Not Call It By That Name,” last modified January 16, 2019, https://www.genderit.org/node/5232/.
  4. “Know the Facts about Women Online,” eSafety Commissioner, accessed February 22, 2021, https://www.esafety.gov.au/women/know-facts-about-women-online.
  5. Plan International, Free to be online? Girls’ and Young Women’s Experiences of Online Harassment (Surrey: Plan International, 2020), 2, accessed February 22, 2021, https://plan-international.org/es/file/46070/download?token=dbMFU3KG.
  6. Pollicy, Alternate Realities, Alternate Internets (Kampala: Pollicy, 2020), 47, accessed February 23, 2021, https://ogbv.pollicy.org/report.pdf.
  7. “Understanding Misinformation, Disinformation and Malinformation” (infographic), Tech Hive Advisory, November, 2020, accessed February 23, 2021, https://techhiveadvisory.org.ng/wp-content/uploads/2020/11/misinformation-844×1024.jpg
  8. Stabilisation Unit, Quick Read-Gender and countering disinformation (London: Stabilisation Unit, 2020), 1, accessed February 23, 2021, https://assets.publishing.service.gov.uk/government/uploads/system/uploads/attachment_data/file/866353/Quick_Read-Gender_and_countering_disinformation.pdf.
  9. Rana Ayyub, “I Was The Victim of a Deepfake Porn Plot Intended to Silence Me,” Life Less Ordinary (blog), HuffPost UK, November 21, 2018, https://www.huffingtonpost.co.uk/entry/deepfake-porn_uk_5bf2c126e4b0f32bd58ba316.
  10. “Gendered Disinformation, Fake News, and Women in Politics,” Council on Foreign Relations (blog), December 6, 2019, https://www.cfr.org/blog/gendered-disinformation-fake-news-and-women-politics.
  11. “The Digital Gender Gap is Growing Fast in Developing Countries,” ITU, accessed February 23, 2021, https://itu.foleon.com/itu/measuring-digital-development/gender-gap/.
  12. “The Gender Gap in Internet Access: Using a Women-Centred Method,” Web Foundation (blog), March 10, 2020 https://webfoundation.org/2020/03/the-gender-gap-in-internet-access-using-a-women-centred-method/.
  13. GSMA, The Mobile Gender Gap Report 2020 (London: GSMA, 2020), 30, accessed February 23, 2021, https://www.gsma.com/mobilefordevelopment/wp-content/uploads/2020/05/GSMA-The-Mobile-Gender-Gap-Report-2020.pdf.
  14. “Internet Shutdowns, Gender, Net Neutrality, and more at the United Nations,” Access Now, June 6, 2017, https://www.accessnow.org/internet-shutdowns-gender-net-neutrality-united-nations.
  15. S. K. Chinmayi and Rohini Lakshané, Of Sieges and Shutdowns (Bangalore: The Bachchao Project, 2018), 36, accessed February 23, 2021, http://thebachchaoproject.org/wp-content/uploads/Of_Sieges_and_Shutdowns_The_Bachchao_Project_2018_12_22.pdf.
  16. “Internet shutdowns in Africa: ‘It is like being cut off from the world’,” Association for Progressive Communications, last updated July 22, 2019, https://www.apc.org/en/news/internet-shutdowns-africa-it-being-cut-world.
  17. Deborah Brown and Allison Pytlak, Why Gender Matters in International Cyber Security (Women’s International League for Peace and Freedom and the Association for Progressive Communications, 2020), 10-12, accessed February 23, 2021, https://www.apc.org/sites/default/files/Gender_Matters_Report_Web_A4.pdf.
  18. General Assembly resolution 48/104, Declaration on the Elimination of Violence against Women, A/RES/48/104 (20 December 1993), available from http://www.un-documents.net/a48r104.htm.
  19. Crystal Dicks and Prakashnee Govender, Feminist Visions of the Future of Work: Africa (Berlin: Friedrich-Ebert-Stiftung, 2020), 8 – 9, accessed February 23, 2021, http://library.fes.de/pdf-files/iez/15796.pdf
  20. Tech Hive Advisory, “Digital Lending: Inside the Practice of LendTechs”, LinkedIn, February 19, 2021, https://www.linkedin.com/posts/tech-hive-advisory_digital-lending-inside-the-practice-of-lendtechs-activity-6768431134297620480-E5zx.
  21. Francis Monyango, “Mobile Money Lending and AI: The Right not to be Subject to Automated Decision Making,” Global Information Society Watch, March 24, 2019, https://www.giswatch.org/node/6177.
  22. Amanda Gouws, “Unpacking the Difference between Feminist and Women’s Movements in Africa,” Conversation, August 9, 2015, https://theconversation.com/unpacking-the-difference-between-feminist-and-womens-movements-in-africa-45258
  23. Karen Beckwith, “Beyond Compare? Women’s Movements in Comparative Perspective,” European Journal of Political Research 34, no. 4 (2000): 437–438, https://doi.org/10.1111/1475-6765.00521.
  24. Sandra Aceng, “Online GBV – Why it’s Still Crucial to Raise Awareness,” Digital Human Rights Lab (blog), December 15, 2020, https://digitalhumanrightslab.org/blog/why-its-still-important-to-create-awareness-about-ogbv/.
  25. “Raising Youth Awareness and Seeking Support for ‘Policies That Favour a Feminist Internet’: Taking Back the Tech With CITAD,” Take Back The Tech, accessed February 23, 2021, https://www.takebackthetech.net/blog/raising-youth-awareness-and-seeking-support-“policies-favour-feminist-internet”-taking-back.
  26. Christoph Stork and Steve Esselaar, When the People Talk: Understanding the Impact of Taxation in the ICT Sector in Benin (Washington DC: Alliance for Affordable Internet, 2019), 3, accessed February 23, 2021, https://1e8q3q16vyc81g8l3h3md6q5f5e-wpengine.netdna-ssl.com/wp-content/uploads/2019/03/A4AI_Benin-Tax-Report_Screen_AW.pdf.
  27. “Here’s Your Guide to Conducting Digital Advocacy,” Pollicy (blog), Medium, September 29, 2020, https://pollicy.medium.com/heres-your-guide-to-conducting-digital-advocacy-5cf9fce92b29
  28. Darina Lynkova, “Women in Technology Statistics: What’s New in 2020?,” Tech Jury (blog), January 22, 2020, https://techjury.net/blog/women-in-technology-statistics/.
  29. “About Us,” WanaData (blog), Medium , April 11, 2019, https://medium.com/wanadata-africa/about-us-a4c53027b716.
  30. Django Girls (website), accessed February 23, 2021, https://djangogirls.org/.
  31. Safe Sisters (website), accessed February 23, 2021 https://safesisters.net/.
  32. Cyberwomen (website), accessed February 23, 2021, https://cyber-women.com/.
  33. Gender and Tech Resources (website), accessed February 23, 2021, https://gendersec.tacticaltech.org/wiki/index.php/Main_Page.
  34. “Internet Freedom Festival,” Civil Rights Defenders, March 13, 2018, https://crd.org/2018/03/13/internet-freedom-festival/